SHINDANO LA WASICHANA KATIKA TEHAMA

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA inawaalika wamafunzi wasichana wote wa Vyuo vikuu nchini kushiriki katika shindano la ubunifu linalohusisha uwasilishaji wa wazo lenye ubunifu Zaidi katika jamii litakalo gusa siku ya WASICHANA NA TEHAMA 2024.

Shindani hili linalenga kumpatia kila mmoja fursa ya kushiriki, kuonesha ujuzi, na kufurahia ubunifu, uvumbuzi na hatimaye kukuza weleledi wa uongozi katika TEHAMA.

SIFA ZA MSHIRIKI

  • Awe mwanafunzi msichana wa chuo kikuu Tanzania.
  • Awe na ujuzi wa msingi wa kutumia programu za usimbaji, (coding) mfano Python na R.
  • Awe na umri kati ya miaka 18 na 24
  • uanachama wa klabu za kidijitali ni sifa ya ziada

Washiriki wanatakiwa kuwasilisha maombi yao kupitia kiungo kifuatacho http://edodoso.gov.go.tz/index.php/824558?newtest=Y&lang=en mwisho wa kutuma maombi ni 12 Machi 2024