TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII 8,900

WIZARA YA AFYA

TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inatekeleza Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii nchini. Kupitia Mpango huu, Serikali imeweka utaratibu wa kuwapata Wahudumu wenye sifa zilizowekwa, kutoa mafunzo na kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika utekelezaji wa afua Jumuishi za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii ambapo Mpango unahitaji Wahudumu wawili (2) yaani Mwanaume na Mwanamke kwa kila Kitongoji/Mtaa.

Katika kutekeleza Mpango huu, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI inawatangazia Wananchi kuwa Mpango huu kwa awamu ya kwanza utaanza katika Mikoa 10 na Halmashauri mbili (2) kwa kila Mkoa kama inavyoonekana katika Jedwali:

MKOANAHALMASHAURIIDADI YA WAHUDUMU (CHWS)
  GEITA1Geita TC224
2Bukombe DC696
 Jumla920
    
  KAGERA1Bukoba MC132
2Biharamulo DC746
 Jumla878
    
  KIGOMA1Buhigwe DC384
2Kakonko DC710
 Jumla1094
    
  LINDI1Lindi MC234
2Lindi/Mtama DC1490
 Jumla1724
    
MBEYA1Mbeya CC362
2Busokelo DC474
  Jumla836
    
  NJOMBE1Makambako TC242
2Njombe TC504
 Jumla746
    
  PWANI1Kibaha TC146
2Rufiji DC334
 Jumla480
    
  SONGWE1Tunduma TC142
2Ileje DC632
 Jumla774
    
  TABORA1Tabora MC586
2Nzega TC380
 Jumla966
    
  TANGA1Handeni TC120
2Tanga City Councils362
 Jumla482
 JUMLA KUU8,900

Aidha, Utekelezaji wa Mpango huu utaendelea kwa awamu katika Mikoa na Halmashauri zote za Tanzania Bara. Wananchi wenye sifa stahiki ndani ya Mikoa 10 iliyooneshwa katika Jedwali hapo awali, wanahimizwa kuomba nafasi za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika Mitaa/Vitongoji vyote ndani ya Halmashauri zao. Maombi yote yawasilishwe kwa Wakurugenzi waHalmashauri, ambao watasimamia zoezi la kuwachagua Wahudumu wenye sifa miongoni mwa waliotuma maombi kwa kuzingatia Miongozo iliyotolewa.

Sifa za waombaji:

Maombi yawasilishwe Ofisi ya Mtendaji wa Kata yakiambatanishwa na:

  1. Barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa kwa mkono na kuwekwa saini ya mwombaji
  2. Nakala ya Cheti cha kuhitimu Kidato cha Nne (Form IV Leaving Certificate);
  3. Picha mbili (2) za Passport Size;
  4. Maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani kamili na namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/namba ya simu ya kiganjani ya Wadhamini wasiopungua wawili (2).
  5. Barua ya uthibitisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa wa eneo analotoka.

Mwisho wa kuwasilisha maombi haya ni wiki mbili (2) tangu tarehe ya kutolewa kwa tangazo hili. Maelekezo zaidi yanapatikana kupitia Ofisi za Watendaji wa Kata husika.

Imetolewa na:

KATIBU MKUU

S.L.P 743 DODOMA

06/04/2024